Rais Ruto ametetea mfumo mpya wa ufadhili vyuo vikuu

  • | Citizen TV
    2,078 views

    Rais William Ruto ametetea mfumo wa ufadhili wa elimu ya juu huku sasa akisema wizara ya elimu itaongeza ufadhili wa elimu na mikopo kwa wanafunzi wasiojiweza. Rais akisema kuwa mabadiliko ya mfumo huu wa elimu ni muhimu ili kuhakikisha wanafunzi wasiojiweza wanamudu kupata elimu. Matamshi ya rais yakijiri wakati ambapo hisia zimeendelea kuhusiana na mfumo mpya wa ufadhili wa elimu kwa kuzingatia mtazamo wa kimapato. Rais alikuwa akizungumza wakati wa hafla ya kufuzu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Eastern Africa Baraton kaunti ya Nandi.