Wanafunzi watatizika kupata fedha kugharamia elimu

  • | Citizen TV
    737 views

    Huku wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu wakitarajiwa kuanza kuripoti vyuoni wiki hii, baadhi ya wanafunzi wamesalia njiapanda baada ya mfumo mpya wa ufadhili kuwalazimu kulipa karo zaidi. Josiah Ongachi kutoka kaunti ya Kisii ni mmoja kati ya maelfu ya wanafunzi waliosalia bila namna baada ya familia kushindwa kupata fedha zinazohitajika. Na kama Chrispine Otieno anavyoarifu, mwanafunzi huyu aliyepata A huenda akashindwa kujiunga na chuo kikuu cha Kenyatta juma hili