Korti yampa Kawira Mwangaza afueni ya muda kuzuia kutimuliwa kwake

  • | Citizen TV
    3,143 views

    Ni afueni ya muda kwa gavana wa Meru Kawira Mwangaza baada ya mahakama kuu kuzuia utekelezwaji wa uamuzi wa kumtimua afisini. Uamuzi huu ukijiri saa chache baada ya maseneta kupitisha hoja ya kumtimuliwa jana usiku. Hata hivyo, kupitishwa kwa hoja ya kumfurusha Gavana Mwangaza, ilishuhudia kizaazaa bungeni, baadhi ya maseneta wakijeruhiwa