Rais Ruto kuzindua rasmi kampeni ya Raila Odinga ya uwenyekiti wa tume ya muungano wa Afrika

  • | Citizen TV
    1,966 views

    Mkuu wa mawaziri na waziri wa maswala ya kigeni Musalia Mudavadi amesema kuwa Kenya iko tayari kuendesha kampeni za Raila Odinga kuwa mwenyekiti wa tume ya muungano wa umoja wa Afrika. Katika kikao cha pamoja na Odinga, mudavadi ameongeza kuwa rais William Ruto atazindua rasmi kampeni hiyo wiki ijayo na kuwataja maafisa serikali watakaozuru mataifa mengine barani Afrika kutafuta uungwaji mkono kwa Odinga