Wakazi wa Meru watoa maoni baada ya kubanduliwa kwa Gavana Mwangaza

  • | KBC Video
    40 views

    Uamuzi wa bunge la seneti la kumng’atua afisini gavana Kawira Mwangaza ambao iwapo utaidhinishwa na mahakama huenda ukamtokomeza kisiasa umepokelewa kwa hisia mseto miongoni mwa wakazi wa kaunti ya Meru. Huku wawakilishi wadi waliopiga kura kumng’atua gavana huyo wakisherehekea kwa densi na nyimbo, baadhi ya wakazi walionekana kuunga mkono hatua ya gavana huyo ya kutafuta haki mahakamani wakidai alihujumiwa kisiasa, huku wengine wakisema anafaa kuondoka ofisini kwa manufaa ya maendeleo ya kaunti. Hizi hapa baadhi ya semi za wakazi hao kuhusu hatua ya bunge la seneti.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News