Maskofu wa kipentekoste wapinga mswada uliopendekezwa wa kudhibiti makanisa

  • | KBC Video
    10 views

    Zaidi ya maaskofu 100 wa makanisa ya kipentekoste kote nchini wametahadharisha bunge dhidi ya kupitisha mswada wa kudhibiti makanisa.Wakiongozwa na mwenyekiti we muungano wa kitaifa wa wahubiri Askofu Stephen Ndicho, maaskofu hao walikosoa pendekezo la kudhibiti makanisa wakisema mchakato wa kuratibu muswada huo hauhusisha maoni ya umma. Walisema mswada huo unalenga hasa makanisa ya kipentekoste bila kuzingatia usawa kwa kupendekeza sheria kali ambazo huenda zikaathiri uhuru wa kuabudu. Maaskofu hao wametoa changamoto kwa serikali kutathmnini upya mswada uliopendekezwa wakisema iwapo utapitishwa huenda ukaleta mgawanyiko miongoni mwa makundi ya kidini humu nchini.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive