Wanaharakati waitaka serikali kurejelea mfumo wa hapo awali wa kufadhili vyuo vikuu

  • | Citizen TV
    314 views

    Utata kuhusiana na ufadhili wa elimu ya vyuo vikuu umeendelea huku wanafunzi zaidi wakisimulia walivyokwama kuendelea na masomo. Haya yanajiri huku wadau wa elimu sasa wakimtaka rais William Ruto kufutilia mbali kamati aliyopendekeza mapema wiki hii kushughulikia utata huu. Na kama Emily Chebet anavyoarifu, shinikizo zimeendelea kurejesha mfumo wa zamani wa ufadhili.