Walemavu wa kusikia waelezea masaibu yao Homa Bay

  • | Citizen TV
    341 views

    Huku ulimwengu ukiendelea kuadhimisha mwezi wa hamasisho kwa wasio na uwezo wa kusikia, wanaoishi na hali hii wanaitaka serikali kutimiza ahadi yake na kutilia maanani maswala yao. Haya yakizungumzwa mwaka mmoja baada ya serikali kuzindua mchakato wa kuhakikisha uwepo wa huduma za matibabu na uchunguzi wa masuala ya afya ya masikio. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, baadhi ya waathiriwa bado wanadai kutelekezwa kwa misingi ya kukosa uwezo wa kusikia.