Kenya yaweka mikakati ya kukabiliana na uhalifu mitandaoni

  • | Citizen TV
    297 views

    Kongamano la pili la wiki nzima kuhusu usalama wa mtandao linaingia siku yake ya pili katika chuo kikuu cha Nairobi. Katika taarifa iliyowasilishwa kwenye vyombo vya habari jumanne, katibu mkuu wa usalama daktari Raymond Omolo amesema kuwa serikali imeweka mikakati ya kuanzisha vituo vya usalama mtandaonikama njia itakayosaidia katika ubunifu wa mtandao na kukabiliana na uhalifu wa mitandaoni.