Maafisa kutoka wizara ya usalama kuhusishwa katika mpango wa usajili wa wakenya kwa bima ya SHA

  • | Citizen TV
    399 views

    Maafisa wa utawala katika wizara ya usalama wa kitaifa wamehusishwa katika mpango wa usajili wa WaKenya katika bima mpya ya afya ya jamii SHA kabla ya uzinduzi wake rasmi wiki ijayo. Maafisa hao watatumia ile mbinu iliyotumika wakati wa usajili wa wakulima milioni 6 katika mpango wa mbolea ya ruzuku. Ushirikiano huu kati ya Wizara ya Afya na usalama unajiri huku serikali ikijiandaa kuanza usajili wa zaidi ya watu milioni 30 katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mpango huu wa afya kwa wote.