Wakazi wa lokesheni ya Sosiana wanadai chifu

  • | Citizen TV
    446 views

    Wanakijiji wa lokesheni ya Sosiana maeneo ya Transmara South wanazidi kulilia serikali kuwatumia Chifu mpya baada ya eneo hilo kuratibiwa kwenye gazeti rasmi ya serikali kaka lokesheni miaka minane iliyopita. Wakizungumza jumapili katika eneo la Sosiana, Wenyeji hao wanasema hatua ya kutokuwa na chifu imelemaza huduma kadhaa za serikali ikiwemo ukosefu wa kupata vitambulisho mapema, kusajiliwa kwa wakongwe miongoni mwa huduma zingine za serikali.Aidha wanasema sehemu hiyo iliyoko Transmara Kusini ni pana mno na huenda wakazi wakazidi kuhangaika zaidi licha ya mahojiano ya kupata chifu mpya kufanyika miaka kadhaa iliyopita.