Seneti yaanza kusikiza madai dhidi ya Mutai

  • | Citizen TV
    896 views

    Bunge la seneti limeanza kusikiza hoja ya kumuondoa gavana wa Kericho Dkt. Erick Mutai baada ya bunge la kaunti kumtimua. Mutai anakabiliwa na tuhuma za kukiuka katiba, kutimia vibaya ofisi yake, kufuja pesa za umma na ubadhirifu wa pesa zilizotolewa kuwafidia waathiriwa wa ajali ya Londiani miongoni mwa tuhuma zingine. Wakili wa kaunti ya Kericho Elias Mutuma ameitaka seneti kusikiza faraghani tuhuma zinazohusiana na dhulma za kijinsia ili kulinda shahidi.