Mradi wa maji unaotumia jua wawafaidi wakazi Isiolo

  • | Citizen TV
    583 views

    Wakazi wa eneo la wabera , kaunti ya Isiolo wamepata afueni kufuatia kuzinduliwa kwa mradi wa maji unaotumia nishati ya jua. uzinduzi wa Kisima kinachosambaza maji kwa kutumia miale ya jua unatarajiwa kupunguza changamoto mbalimbali kama ukosefu wa maji kwa maeneo yaliyoko mbali. Zaidi ya watu elfu sita katika eneo hilo wamefaidika na mradi huo ambao pia umepunguza gharama ya umeme na hivyo kutoa nafasi ya utumizi wa rasilimali za kaunti kwenye miradi mingine.