Wakaazi wa Tharaka walalamikia hali mbaya ya barabara kuu ya Tunyai -Nthaara - Marimanti

  • | Citizen TV
    730 views

    Wakaazi eneo la Tharaka wanamtaka Gavana wa Kaunti ya Tharaka Nithi Muthomi Njuki kukamilisha ujenzi wa barabara kuu ya kutoka Tunyai -Nthaara - hadi Marimanti. Ujenzi wa barabara hiyo ulianza miaka Saba iliyopita wakati wa muhula wa kwanza wa Gavana Njuki ambapo ni Kilomita 3 pekee zilizojengwa. wakazi hao wamegadhabishwa na hali mbaya ya barabara hiyo ya Kilomita 20.Aidha waliwafukuza baadhi ya maafisa wanaosemekana kutoka Kwa serikali ya Kaunti ambao walitaka kubomoa bango la ujenzi wa barabara hiyo eneo la Nthaara.