Uchaguzi wa rais wa 2024 unatoa ishara ya kuwepo ushindani mkali kati ya wagombea wawili

  • | VOA Swahili
    500 views
    Fursa mbalimbali zilizowasilishwa na vyama vikuu viwili – Demokratic na Republican – vina uhakika kuwa rais ajaye atakuwa anatokana na chama kimoja wapo kati ya hivyo, kama ilivyokuwa kwa marais wote tangu 1856. Utawala wa mfumo wa vyama viwili unaweza kuonekana ni kitu cha ajabu. Katiba ya Marekani haielezi chochote kuhusu vyama vya siasa, na George Washington – yeye mwenyewe rais wa kwanza na pekee kuchaguliwa bila ya kuwakilisha chama cha siasa – alitahadharisha dhidi ya vyama katika hotuba yake ya kuliaga taifa. Hii hapa ripoti kamili ikisomwa na mwandishi wa VOA Kennes Bwire... #uchaguzi #marekani #republikan #demokratiki #independent #voa #voaswahili