Msigwa aeleza bado anaimani timu ya Tanzania itafuzu AFCON 2025

  • | VOA Swahili
    58 views
    Geron Msigwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo wa kufuzu kuingia kwenye michuano ya Afcon 2025 kati ya Taifa Stars -Tanzania na timu ya DRC Leopard kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa mjini Daressalaam Tanzania. Baada ya mchezo Katibu wa wizara hiyo Gerson Msigwa ameelezea kutoridhishwa na matokeo hayo huku akionyesha imani juu ya timu hiyo kufuzu fainali za AFCON 2025 zitakazofanyika nchini Morocco. Timu ya Taifa ya Soka ya Tanzania, Taifa Stars imepoteza mchezo wa marejeano wa kufuzu fainali za AFCON 2025 dhidi ya DR Congo kwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam. Mabao ya Congo yamefungwa na mshambuliaji Meshack Elia katika dakika za 88 na 90+, nyota huyo akiitumikia Young Boys ya Uswisi katika ngazi ya klabu. Licha ya kupoteza mashabiki wa Stars wamezungumzia mchezo huo wakionyesha ilipokosea. Hadi sasa kwenye msimamo wa kundi H, linaongozwa na DR Congo wenye pointi 12 ambao tayari wamefuzu kwenye fainali hizo, Tanzania (Taifa Stars) nafasi ya pili ikiwa na pointi 4, Guinea nafasi ya tatu pointi 3, Ethiopia ikishika mkia ikiwa na pointi 1. #tanzania #afcon2025 #drc #naibuwaziri #hamismwinjuma #daressalaam #benjaminmkapa #uwanja