Majimbo hayo ambayo ni maarufu kama ‘Swing States’ ni muhimu kushinda kuingia White House mwaka 2024.
Majimbo haya yanayoshindaniwa yanashuhudia kampeni kali za kisiasa na za gharama, na wapiga kura wake wanaushawishi mkubwa katika uchaguzi huo.
Kwa hivyo hili linafanyika vipi?
Majimbo mengi zaidi yanatabirika kuwa mekundu au bluu (Republikan au Democratic), hivyo chaguzi zao hazina ushindani. Lakini katika swing states, matokeo ya uchaguzi yanaweza kuelemea upande wowote.
Mgombea anahitaji kura za wajumbe 270 kati ya 538 kushinda urais, kawaida kuna majimbo ambayo mshindi anachukua kura zote za wajumbe. Swing states hutoa kura za maamuzi, na kuwaruhusu wagombea kuvuka kizingiti kilichowekwa.
Mwaka huu, Arizona, Georgia, Michigan, Nevada, North Carolina, Pennsylvania na Wisconsin wana uamuzi nani ataingia White House. Kati yao, kuna kura za wajumbe 93 ambazo zinaweza kuelemea upande mwekendu au bluu.
Majimbo haya yana kura chache za wajumbe kwa sababu ya uwiano wa karibu kati ya wapiga kura wa Republikan na Demokrat. Kuhama kwa idadi ya watu na ushindani wa maoni kati ya maeneo ya mijini na vijijini unafanya matokeo hayatabiriki.
Endelea kusikiliza...
#swingstates #marekani #uchaguzimkuu2024 #warepublikan #wademokratiki #wapigakura