Mfumo wa uchaguzi wa Marekani unategemea kura za wajumbe hutumika kumpa ushindi rais

  • | VOA Swahili
    112 views
    Baada ya kila chama kumteua mteule wa kuwania urais, mteule huyo kimkakati humchagua mgombea mwenza kwa ajili ya uchaguzi mkuu. Timu huanza kazi kwa bidii kwa kampeni ya matayarisho kwa ajili ya siku ya mwisho ya upigaji kura hapo Novemba 5, Jumanne ya kwanza ya mwezi Novemba. Siku ya uchaguzi, wapiga waliojiandikisha wanakwenda katika vituo vya kupigia kura kumchagua mgombea uraia wa chama chao. Rais kimsingi ataamuliwa na mfumo maarufu unaoitwa kura za wajumbe. Kura za wajumbe inaundwa na wawakillishi, au wapiga kura, ambao wametengwa kulingana na matokeo ya kupiga kura katika kila jimbo. Majimbo yenye idadi kubwa ya watu wana wapiga kura wengi zaidi. Majimbo yenye idadi ndogo ya watu yana wapiga kura wachache. Kushinda urais, mgombea lazima apate wingi wa kura za wajumbe kiasi cha kura 270. Wapiga kura halafu wanapiga kura zao mwezi mmoja baadaye. Lakini rais mpya hachukui madaraka mpaka atakapoapishwa mwishoni mwa mwezi Januari. #kurazawajumbe #electoralcollege #rais #uchaguzimkuu2024 #voa #voaswahili