'...Uamuzi uliochukuliwa haukuwa na ukabila...'

  • | VOA Swahili
    631 views
    Rais wa Kenya William Ruto Ijumaa alimteua waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki kuwa naibu wake mpya, siku moja baada ya baraza la Seneti kupiga kura ya kumtimua naibu wake wa zamani, Rigathi Gachagua.⁣ “Nimepokea ujumbe kutoka kwa rais, kuhusu kuteuliwa kwa Profesa Kithure Kindiki kushika nafasi hiyo ambayo imetokea afisini,” Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula alisema Ijumaa, akiwahutubia wabunge mjini Nairobi.⁣ Gachagua, ambaye alikanusha mashtaka yote dhidi yake wakati wa kesi ya kuondolewa madarakani, alimuunga mkono Ruto katika ushindi wake wa 2022 na kusaidia kupatikana kwa kura nyingi kutoka eneo lenye wakazi wengi la kati mwa Kenya.⁣ Lakini katika miezi ya hivi karibuni , Gachagua amezungumza kuhusu kutengwa, huku kukiwa na taarifa zilizoenea kwenye vyombo vya habari kuwa ametofautiana na Ruto wakati miungano ya kisiasa ikibadilika.⁣ Kindiki, mshirika wa karibu wa Ruto, ameshikilia wadhifa wa wizara ya mambo ya ndani katika kipindi chote cha miaka miwili ya Ruto kama rais.⁣ Hapo awali aliwahi kuwa seneta wa Kaunti ya Tharaka Nithi na alikuwa mgombeaji mkuu kuwa mgombea mwenza wa Ruto wakati wa uchaguzi wa 2022.⁣ Baadaye Bunge litalazimika kupiga kura kuidhinisha uteuzi wa Kindiki kabla ya kuapishwa.⁣ ⁣ ⁣ #Kenya #seneti #gachagua #kindiki #voa #voaswahili