Viongozi wa dini wapinga mswada

  • | Citizen TV
    2,904 views

    Umati wa wakenya wamejitokeza katika jumba la KICC jijini Nairobi kuwasilisha maoni yao kuhusu mswada unaopania kuongeza muhula wa Rais kutoka miaka mitano hadi miaka saba. Mswada huo unalenga kufanyia katiba marekebisho ili kuwawezesha viongozi wote wanaochaguliwa kuweza kuhudumu mihula miwili ya mika saba kila moja badala ya miaka mitano. Tayari baadhi ya wakenya , viongozi wa dini na vyama vya kisiasa vimepinga mswada huo. Mswada huo uliowasilishwa na seneta wa Nandi Samson Cherargei ni wa pili wa aina hiyo. Cherargei anasema kuwa miaka 7 itawaruhusu viongozi tutekeleza ahadi zao kwa wananchi.