Takriban watu 51 wafariki kutokana na mafuriko Uhispania

  • | VOA Swahili
    80 views
    Wizara ya ulinzi na picha za polisi zimewaonyesha wafanyakazi wa huduma za dharura wakikagua nyumba zilizokumbwa na mafuriko na kuwaokoa watu kwenye mji wa Utiel. Dazani za video zilizobandikwa kwenye mitandao ya kijamii usiku zimewaonyesha watu wakiwa wamekwama kwenye maji ya mafuriko, wengine walipanda kwenye miti kuepuka kusombwa na maji. Carlos Mazon, mkuu wa mji wa Valencia aliwaambia waandishi wa habari baadhi ya watu bado wametengwa katika maeneo ambayo hayafikiki. Hata hivyo huduma za dharura katika eneo hilo zimewasihi raia kuepuka safari za barabarani na kufuatilia taarifa nyingine kutoka vyanzo rasmi. - Reuters