Rais Ruto adai wakosoaji wa SHA ni wale walioshiriki ufisadi NHIF

  • | K24 Video
    19 views

    Saa chache baada ya ripoti ya mkaguzi mkuu wa mahesabu serikalini Nancy Gathungu kuweka bayana kuwa serikali haimiliki teknolojia inayotumika na bima ya SHA, Rais William Ruto amepinga madai kuwa fedha za teknolojia hiyo zinalipwa na serikali. akizungumza wakati wa mazishi ya mbunge wa Malava Malulu injendi, Ruto amewalimbikizia lawama wale aliowataja kama matapeli walionufaika chini ya bima ya NHIF kwa madai ibuka kuhusu SHA.