Abiria aibiwa Safarini

  • | Citizen TV
    26,997 views

    Abiria mmoja anayeishi Diani kaunti ya Kwale analilia haki baada ya kudai kuwa alipulizwa dawa za kulala na baadaye kuibiwa mali yake alipokua akisafiri kutoka Nairobi kuelekea Mombasa. Dalila Omondi alikua ameabiri basi la kamouni ya Mash tarehe 14 mwezi huu na baadaye kujipata katika hospiitali kuu ya Pwani mjini Mombasa akipokea matibabu. Anasema juhudi zake za kupata majibu kutoka kampuni ya Mash kuhusu kilichomfanyikia hazujazaa matunda.