Askofu mkuu Muheria ataka vitendo badala ya vibwagizo vya kasuku

  • | K24 Video
    172 views

    Askofu mkuu wa kanisa katoliki dayosisi ya Nyeri, Anthony Muheria, ameiomba serikali kwa dharura itoe fedha zilizocheleweshwa kwa hospitali za dini, chini ya hazina ya bima ya afya ya kitaifa (NHIF) na mamlaka ya afya ya kijamii (SHA). Muheria ameishutumu serikali kwa kutotimiza ahadi yake baada ya kufanya makubaliano na hospitali za dini kukubali bima mpya ya afya ya jamii, taifa care, ikiahidi kulipa madeni yote ya NHIF. Hospitali za dini na muungano wa hospitali za mashinani na za kibinafsi zilikuwa zimekataa kusaini mikataba ya bima mpya.