Askofu Mkuu wa kanisa la Kianglikana Ole Sapit ataka Gachagua asihujumiwe

  • | Citizen TV
    2,780 views

    Askofu mkuu wa kanisa la kianglikana nchini Jackson Ole Sapit amelitaka bunge la seneti kumfanyia haki naibu rais Rigathi Gachagua, atakapofika mbele ya bunge hilo wiki hii, kujitetea dhidi ya hoja ya kumuondoa ofisini. Sapit wakati huo huo amesema muda umewadia kwa wanasiasa kufanyiwa ukaguzi wa mali kama watumishi wa umma ili kubaini wale wanaohusika na ubadhirifu wa fedha za umma kwa kuwa wafisadi.