Askofu Timothy Ndambuki asema taifa linaendelea kudidimia kwenye sekta ya demokrasia

  • | Citizen TV
    501 views

    Askofu mkuu wa kanisa la ABC Afrika mashariki na kati Dkt. Timothy Ndambuki ameelezea wasiwasi wake kuwa taifa linaendelea kudidimia kwenye ukabila na kutishia demokrasia na umoja wa taifa hili. Askofu Ndambuki amesema kuendelea kushuhudiwa kwa visa vya utekaji nyara na cheche za ukabila kutoka kwa viongozi kunaliweka taifa hili kwenye hatari.