Assange aachiwa huru

  • | BBC Swahili
    807 views
    Jumanne Julian Assange alianza safari yake ya kurudi nyumbani Australia, baada ya kufikia makubaliano na mamlaka za Marekani. Mwanzilishi huyo wa WikiLeaks ametumia miaka mitano iliyopita gerezani nchini Uingereza. Assange alishtakiwa kwa kula njama ya kupata na kufichua taarifa za ulinzi wa taifa, baada ya tovuti ya Wikileaks kuchapisha rekodi za siri za kijeshi za Marekani. Kulingana na CBS, Assange hatatumikia muda wowote chini ya ulinzi wa Marekani kama sehemu ya makubaliano na wizara ya sheria na atapewa msamaha kwa muda aliokaa jela nchini Uingereza. #bbcswahili #australia #Wikileaks Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw