Baadhi wa viongozi wa Azimio wa mshutumu Raila vikali, baada ya kuungana serikali ya Kenya Kwanza

  • | NTV Video
    2,181 views

    Hatua ya Kinara wa ODM Raila Odinga ya kuungana na serikali ya Kenya Kwanza imesutwa vikali na baadhi ya viongozi wa Muungano wa Azimio wa hivi punde akiwa ni Gavana wa kaunti ya machakos Wavinya Ndeti na naibu wake Francis Mwangangi ambao wamelalamika kuwa Odinga amewasiliti Wakenya kwa kuungana na watu wanaodaiwa kusababisha vifo vya vijana wa Gen Z waliokuwa wakiandamana Kuipinga serikali. Wamesema haya eneo la katangi walipozindua barabara ya kilomita 42 kutoka Katangi kuelekea Kithimani eneo bunge la Yatta. Kulingana na Mwangangi, Kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka anastahili kuheshimiwa kwani ametangaza msimamo wake na kwamba ana nafasi bora zaidi kuwa rais wa Kenya katika uchaguzi mkuu ujao.

    Subscribe to NTV Kenya channel for latest Kenyan news today and everyday. Get the Kenya news updates, discussions and other exciting shows.

    Website: ntv.nation.co.ke || Paper: Daily Nation || Twitter: @ntvkenya || Facebook: NTV Kenya || Instagram: NTV Kenya