Baadhi ya wabunge wataka uchunguzi kuhusu visa vya utekaji nyara

  • | KBC Video
    44 views

    Baadhi ya wabunge wanaomuunga mkono aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagua sasa wanataka tume huru ya uchunguzi ibuniwe kuchunguza visa vya madai ya utekaji nyara na unyakuzi wa ardhi. Wakiongozwa na Seneta wa Kiambu Karungo Thang'wa wabunge hao wanasema polisi hawawezi kuaminiwa kutegua kitendawili cha visa vilivyoripotiwa vya utekaji nyara wa watu wanaodhaniwa kuwa wakosoaji wa serikali na hivyo ipo haja ya kuwa na tume ya uchunguzi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive