Skip to main content
Skip to main content

Baadhi ya wakazi Nyamira wahamasisha vijana kujitokeza kusajiliwa kura

  • | Citizen TV
    95 views
    Duration: 1:37
    Baadhi ya wakazi wa kaunti ya Nyamira wamezuru vijiji mbalimbali kuwahimiza vijana kujitoteza na kujisajili kuwa wapiga kura, baada ya kaunti hiyo kuorodheshwa kati ya zile zilizoandikisha wapiga kura wachache zaidi nchini wiki jana. Wakizungumza walipozuru vijiji mbalimbali kule Mugirango Kaskazini, wakazi hao wamesema kujisajili na kupiga kura ndiyo njia mwafaka ya kusukuma ajenda ya mageuzi na kuwachagua viongozi bora nchini. Aidha wakazi hao wameiomba serikali kuwasajili vijana na kuwapa vitambulisho kwa wakati, ili kuwawezesha kujiandikisha kama wapiga kura.