Biden asema: '... Huwezi kuipenda nchi yako pale tu unaposhinda, ...'

  • | VOA Swahili
    407 views
    Rais Joe Biden Alhamisi aliwasihi Wamarekani kukubali matokeo ya uchaguzi wa rais wa Jumanne, ambapo Rais wa zamani Donald Trump alimshinda mrithi wa Biden, Makamu Rais Kamala Harris. Ameahidi kukabidhi madaraka kwa Trump, ambaye anachukua hatamu za uongozi, ambaye aliwashawishi wafuasi wake kuandamana hadi kwenye jengo la bunge wakati wajumbe walipokuwa wanarasimisha ushindi wa Biden 2020. Rais Joe Biden jana Alhamisi aliahidi kukifanya kipindi cha mpito cha mrithi wake Rais mteule Donald Trump kuwa na utaratibu mzuri. Pia ameomba umoja baada ya kushindwa kwa mgombea aliyempendelea, Makamu Rais Kamala Harris. Joe Biden, Rais wa Marekani: “Watu wamepiga kura na kuchagua viongozi wao, na walifanya hivyo kwa amani. Sisi tuko katika demokrasia, nia ya watu siku zote ndiyo inashinda.” Trump, katika hotuba yake ya ushindi siku moja kabla, pia alisisitiza umoja, wakati akielezea njia ya wazi miongoni mwa wapiga ambayo imempa yeye ushindi mzuri. #rais #donaldtrump #kamalaharris #wafuasi⁣⁣ #voaelections ⁣⁣⁣⁣⁣⁣⁣ #voaelections2024