Burundi yawarejesha nyumbani wanajeshi wa DRC

  • | BBC Swahili
    607 views
    Serikali ya Burundi imeanza rasmi mchakato wa kuwarejesha nyumbani wanajeshi na maafisa wa polisi wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ambao walikimbia baada ya wasi wa M23 kuteka maeneo kadhaa ya mashariki mwa Congo. Tayari wanajeshi 60 wamefikishwa mahakamani huko Lubero Kaskazini mwa mji wa Goma, kwa kutoroka mapigano Mashariki mwa DRC. Mamia ya maafisa hao walikimbilia Burundi kama wakimbizi lakini walipewa hifadhi katika kambi maalum iliyoko katika mji wa Muravya, kilomita 50 kutoka mjini Bujumbura.