Chombo cha Utafiti China charudi kutoka mwezini

  • | BBC Swahili
    849 views
    Picha zilizotolewa na shirika la utangazaji la serikali nchini China zinaonyesha chombo cha utafiti mwezini kilivyorudi duniani baada ya safari ndefu ya karibu miezi miwili. Chang'e-6 ilitua katika jangwa huko Inner Mongolia siku ya Jumanne, kikiwa na sampuli za kwanza kabisa kutoka upande wa mbali usiofahamika katika mwezi. China ndiyo nchi pekee ambayo imewahi kutua upande wa mbali wa Mwezi. Wanasayansi wanasubiri kwa hamu kwani sampuli zinaweza kujibu maswali muhimu kuhusu jinsi sayari zinavyoundwa. #bbcswahili #sayari #angazambali Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw