Dhamana zarundikana katika mahakama ya Nyahururu

  • | Citizen TV
    373 views

    Mahakama ya Nyahururu imesema kwamba mamilioni ya pesa bado haijakusanywa na wadhamini baada ya washtakiwa kuwasilisha dhamana na kesi zao kukamilishwa.Kwa mujibu wa Hakimu Mkuu Evans Keago, waliowasilisha dhamana tangu mwaka 1996 hadi sasa bado hawajazichukua akisema kuwa imekuwa vigumu kuwafikia baadhi ya wadhamini hata baada ya kuwatambua na kuzitaka familia za wahusika ambao kesi zao zilikamilika wafike mahakamani