Diamond awabwaga waNigeria katika tuzo za Trace

  • | BBC Swahili
    1,646 views
    Kisiwani Zanzibar nchini Tanzania Jumatano usiku kulikuwa na tuzo za muziki barani Afrika za Trace. Tuzo hizo zilileta pamoja wasanii na wadau wa tasnia hiyo kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina yao na kusaidia kukuza talanta za muziki kutoka bara hili. Baadhi ya wasanii waliohudhuria ni kama vile Yemi Alade na Rema kutoka Nigeria, Diamond Platnumz wa Tanzania, Bien wa Kenya, Joshua Baraka wa Uganda na wengine wengi. Hata hivyo tuzo hizo zilikatishwa kutokana na maji kujaa karibu na jukwaa.