- 312 viewsDuration: 1:27Waziri wa afya Aden Duale ameweka bayana nia ya serikali kuweka mikakati zaidi kuepusha taifa na visa vya akina mama au watoto kuaga dunia katika vyumba ya uzazi hospitalini. Akizungumza katika eneo la Rumuruti Kaunti ya Laikipia alikozindua ujenzi wa hospitali PCEA Rumuruti, Duale alidokeza kuwa viongozi akina mama wanatarajiwa kuwa mstari wa mbele katika kubuni Mbinu za kuhamasisha jamii kuhusu afya ya Uzazi.