Fahamu kuhusu hali ya kibinadamu DRC katika Dira ya Dunia TV

  • | BBC Swahili
    16,654 views
    Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamekutana katika makao makuu ya umoja wa mataifa wakiwa na matumaini ya kuepusha kuongezeka zaidi kwa mzozo unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wamekuwa wakipiga hatua katika eneo la kusini kuelekea mji wa Uvira, ambao unapakana na mpaka wa Burundi, tangu walipouteka mji mkuu wa jimbo la Bukavu mwishoni mwa juma.