Fahamu kwa nini makaburi Tanzania yako hatarini

  • | BBC Swahili
    1,484 views
    Takriban watu milioni 15 katika nchi zinazoendelea hupata riziki zao kwa ukusanyaji wa vyuma chakavu, ambavyo huongezewa thamani kwa kuchakatwa na kutumika kama malighafi muhimu katika sekta ya ujenzi na viwanda. Lakini sasa baadhi ya watu katika mji wa Morogoro nchini Tanzania wamejikuta kwenye wakati mgumu baada ya misalaba iliyokuwa kwenye makaburi ya wapendwa wao kungolewa ili kuuzwa kama vyuma chakavu.