Familia 90 zinazoishi katika nyumba za teleposta Makande kaunti ya Mombasa zimesalia bila makao

  • | K24 Video
    8 views

    Familia 90 zinazoishi katika nyumba za teleposta makande kaunti ya Mombasa zimesalia bila makao baada ya kufurushwa kwa kile kinachodaiwa ni deni la kodi la shilingi milioni 25. Wapangaji hao ambao baadhi wameishi kwa nyumba hizo kwa zaidi ya miaka 30 wamedai hawakupewa ilani ya kuhama huku wakiitaka serikali iingilie kati kutatua mzozo huo ambao umewaacha zaidi ya watu 300 wakiwemo wanafunzi na wazee bila makao