- 2,258 viewsDuration: 3:27Familia moja katika eneo la Uthiru hapa Jijini Nairobi inadai haki kufuatia kifo cha binti yao aliyeaga dunia alipokuwa akijifungua katika hospitali moja mtaani Kangemi. Kulingana na familia ya Faith Binzali mwenye umri wa miaka 26, msichana huyo alifariki kufuatia utepetevu wa madaktari baada ya upasuaji katika kituo cha afya cha St Joseph the worker Catholic. Upasuaji wa maiti ulionyesha kuwa alifariki kwa kukosa hewa ya kutosha kwenye ubongo..marehemu amemwacha mtoto mchanga kama anavyotuarifu Franklin Wallah