- 65,510 viewsDuration: 3:07Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, na mkosoaji wa serikali ya Tanzania Humphrey Polepole, amevamiwa na kuchukuliwa na watu wasiojulikana, familia yake imethibitisha. Ndugu wa Polepole wameambia BBC kuwa tukio hilo la kuvamiwa na kutekwa kwa ndugu yao kumetokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Oktoba sita nyumbani kwake jijini Dar Es Salaam. BBC imezungumza na kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema jeshi linafuatilia taarifa hizo.