Familia za waathiriwa wa Shakahola zazidi kusubiri mashtaka

  • | Citizen TV
    406 views

    Familia za wahanga wa mauaji ya shakahola zitalazimika kusubiri zaidi kabla ya zoezi la kuwatambua wapendwa wao kukamilika. Mwanakemia mkuu wa serikali amesema kuwa gharama ya kupata vifaa na vipimo pamoja na taratibu za ununuzi wa vifaa hivyo zimechelewesha zoezi hilo kwa miaka miwili sasa. Na kama anavyoarifu francis mtalaki, mchakato huu unaogharimu mamilioni ya fedha huenda ukalazimu baadhi ya familia kutoa upya sampuli za DNA.