Shambulizi la wanamgambo katika hoteli laua idadi ya watu isiyojulikana

  • | VOA Swahili
    570 views
    Bomu la kwenye gari lilipuka Jumanne katika hoteli moja mjiniBeledweyne, katikati mwa Somalia, na kusababisha shambulizi lawanamgambo lililodumu kwa saa kadhaa na kuua idadiisiyojulikana ya watu. Majeshi ya Somalia yaliendelea na juhudi za kuwafurushawashambuliaji Jumanne jioni baada ya mapigano makali. Hoteli ya Cairo inatumiwa na viongozi wa kijadi na maafisa wajeshi ambao wanahusika na uratibu wa mashambulizi ya serikalidhidi ya kikundi cha wanamgambo wa al-Shabaab. Kikundi cha al-Shabaab chenye uhusiano na al-Qaida kilidaikuhusika na shambulizi hilo. Beledweyne, iko kiasi cha kilometa 335 kaskazini mwa mjimkuu, Mogadishu, ni mji mkuu wa mkoa wa Hiran na eneo lakimkakati katika kampeni inayoendelea dhidi ya al-Shabaab.(AP) #somalia #alshabaab #voa
    shabaab