Familia za watu wanne waliofariki kwenye mkasa wa moto Toi zaendelea kuomboleza

  • | Citizen TV
    1,275 views

    Wafanyabiashara wanaohudumu soko la Toi, mtaani Woodley hapa Nairobi wameendelea kukadiria hasara baada ya moto kuteketeza mali yao hapo jana. Huku wengine wakifika kuhesabu hasara, Familia zilizowapoteza jamaa sasa zinadai haki kwa kile wanasema ni utepetevu wa kaunti. Familia ya Kevin Ochieng pamoja na shemejiye Janet Kweyu wanasema ni lazima kaunti ibebe mzigo kwani ilishindwa kudhibiti moto kwa muda muafaka.