Gachagua adai kuna njama ya kumng’atua mamlakani Jaji mkuu Martha Koome

  • | K24 Video
    1,496 views

    Aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua anadai kuna njama ya kumng’atua mamlakani ,jaji mkuu Martha Koome na majaji wa mahakama ya juu. Gachagua amedokeza kuwa rais Ruto ana njama ya kuwateua majaji wa mahakama ya juu watakaoshawishika kwa urahisi hasa kuhusiana na uchaguzi mkuu wa mwaka 2027. Gachagua ameikashifu serikali kwa kile alichokitaja kama njama ya kuhakikisha wakazi wa eneo hilo hawaungani kabla ya uchaguzi ujao