Gachagua avurugwa Nyandarua

  • | Citizen TV
    10,547 views

    Hafla ya maombi iliyokuwa inahudhuriwa na aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua ilivurugwa kwa muda baada ya jamaa anayedaiwa kuwa afisa wa polisi kurusha gesi ya kutoa machozi. Kufuatia vurumai hii, Gachagua amemlaumu Rais William Ruto, akidai kuwa anatumia idara za usalama kuvuruga vikao vyake. Na kama anavyoarifu kamau mwangi, hii ni mara ya pili kwa kikao cha gachagua kuvurugwa katika kipindi cha mwezi mmoja.