Gachagua, Eugene na Kalonzo wasema watashirikiana kisiasa

  • | Citizen TV
    9,679 views

    Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na Eugene Wamalwa wa dap-k wameahidi kushirikiana kumuondoa Rais Ruto uongozini ifikapo mwaka wa 2027. Gachagua akisistiza kwamba chama chake ki-njiani na kwamba uzinduzi wake utatifua kivumbi katika siasa za nchi. Aliyekuwa waziri wa masuala ya ndani Fred Matiangi naye aliwakilishwa na seneta wa Kisii Richard Onyonka kwenye mkutano huu