Serikali ya kaunti ya Nairobi imekanusha madai kwamba wanawake wengi waliojifungua wanazuiliwa katika hospitali za umma baada ya kushindwa kulipa bili za matibabu, ikisema kumekuwa na ucheleweshaji katika shughuli ya kutoa msamaha wa malipo hayo. Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja, ambaye alifika mbele ya kamati ya afya ya bunge la seneti kujibu maswali kuhusu changamoto za miundombinu ya kiafya katika kaunti hiyo, alisema upo mwongozo wazi wa msamaha wa ada za matibabu huku akiwahimiza wakazi kujisajili kwa halmshauri ya afya ya jamii SHA.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive