Gavana wa Homa Bay aitaka serikali kuimarisha usalama ziwani Victoria

  • | Citizen TV
    330 views

    Gavana wa kaunti ya Homa bay Gladys Wanga ameitaka serikali kuu kuimarisha usalama katika ziwa Victoria ili shughuli za uvuvi zisitatizike. Akizungumuza katika ufuo wa Ngeri eneobunge la Suba, Wanga alisisitiza kuwa usalama ziwani ndiyo njia pekee ya kuimarisha sekta ya uvuvi. Kwenye hafla hiyo, serikali ya kaunti ya Homa Bay ilitoa vifaa vya uvuvi vya thamani ya shilingi milioni 30 ili kupiga jeki sekta hiyo.