Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara

  • | VOA Swahili
    7 views
    Ghana inakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara. Baadhi ya waandishi wa habari wana matumaini ya kukabiliana na hali hiyo kwa kutoa ripoti sahihi.⁣ ⁣ Mradi wa Media Foundation for West Africa⁣ ⁣ Kwaku Asante anaongoza timu ya waandishi wa habari wa kuhakiki ukweli, Fact-Check Ghana, mradi wa Media Foundation for West Africa, wenye makao yake katika mji mkuu, Accra.⁣ ⁣ Timu hiyo ina kazi ngumu ya kupambana na habari potofu na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kawaida.⁣ ⁣ Asante anasema yeye na wanahabari wenzake wana kazi kubwa ya kufanya kuhusu changamoto hiyo.⁣ ⁣ Kiongozi wa Timu ya Fact Check⁣ ⁣ Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact Check Ghana anasema:⁣ ⁣ “Kuna taarifa nyingi potofu huko nje. Ukiamka asubuhi unakuta kuna mambo mengi yanayoulizwa. Je, unaweza kuliangalia hili kwa ajili yetu? Je, hizi ni taarifa sahihi? Je, hii ni kweli? Kuna yeyote wa kutusaidia? Kisha tunafika na kusema, “ndiyo, tumeichunguza. Huu ndio ukweli. Hii si sahihi, na hii ni taarifa sahihi.”⁣ ⁣ Kuhakiki ukweli, ni kazi ambayo Asante anaipenda, kwa miaka mitano iliyopita, alifanya kazi kuwajuza raia wa Ghana na taarifa sahihi.⁣ ⁣ Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact-Check Ghana asema: “Inanipa furaha kubwa kujua kwamba unafanya kitu ambacho kinaleta matokeo mazuri na ushawishi wa moja kwa moja kwa watu, kwa sababu habari za uongo zinaweza kuwa na athari mbaya sana, tizama kipindi cha Covid 19 ambapo kulikuwa na mtiririko wa habari za uongo.”⁣ ⁣ Ripoti ya Isaac Kaledzi, VOA, Accra, Ghana.⁣ ⁣ ⁣ #ghana #factcheck #factchecking #voa #uchunguzi #uhakiki #habaripotofu #accra #waandishi - - - - - VOA Swahili inarusha matangazo ya Duniani Leo kupitia Tovuti yetu na jukwaa la Facebook Jumatatu hadi Ijumaa tukikuletea habari mbalimbali za siasa na uchambuzi kwa lugha ya Kiswahili. Tembelea tovuti yetu voaswahili.com/duniani-leo na Makala Maalum ya Jarida la Wikiendi. Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu. Matangazo yetu yanasambazwa kupitia satellite, cable, FM na MW, na and kupitia mtandao wa vituo vya matangazo vya washirika wetu takriban 3000. Tangu kuanzishwa mwaka 1942, Sauti ya Amerika imeendelea na azma yake ya kutoa habari za kina na kuwaambia wasikilizaji wake ukweli. Tangu kipindi cha Vita Vya Pili vya Dunia, Vita Baridi, Vita dhidi ya ugaidi wa kimataifa, na juhudi za ukombozi duniani kote hivi leo VOA imekuwa mfano katika kutekeleza kanuni za vyombo vya habari huru. Jiunge na VOA Swahili: » Tembelea Tovuti Yetu: https://bit.ly/3PtyNWc »Angalia Video Zaidi za VOASwahili: https://bit.ly/3TNTiiI »Pakua VOA+ katika vifaa vya Apple : https://bit.ly/VOAPlus »Download VOA+ katika vifaa vya Android https://bit.ly/3KykriI »Tembelea Tovuti yetu: https://www.voaswahili.com/ »Upende ukurasa wetu wa Facebook: https://www.facebook.com/voaswahili »Tufuatilie katika Instagram: https://www.instagram.com/voaswahili »Tufuatilie katika X: https://twitter.com/voaswahili »Tufuatilie katika YouTube: https://www.youtube.com/@VOASwahili